Thursday, September 17, 2015

UMOJA NI USHINDI 2015

Ahsanteni sana ndugu wananchi wa Pemba kwa kuja kwa wingi kwenye uwanja wa Chokocho Black Magic kumsikiliza mgombea urais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein leo hii 18.Sept 2015.

 
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Ali Mohamed Shein akiwahutubia maelf ya wananchi waliofurika kupita kiasi kwenye Uwanja wa Chokocho Black Wizard kwenye mkutano wa kampeni leo hii tarehe 18 Sept 2015
 
 
 
Mgombea urais wa Zanzibar kwa CHAMA CHA MAPINDUZI dr. Ali Mohamed Shein akizungumza na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Ng. Vuai Ali mara baada ya kuwasili Uwanja wa Gombani ya Kale leo hii Pemba.
Mgombea Urais Dr Ali Mohamed Shein akiowaonesha Katiba ya CCM wananchi waliohudhuria kwenye mkutano
Mgombea Urais Dr Ali Mohamed Shein akiwahutumia maelf ya wananchi wa Pemba waliokuja kusikiliza sera zenye kutekelezeka za Chama Cha Mapinduzi katika uzinduzi wa kampeni Pemba.

DK. SHEIN:TUTAWANYOA KIPARA WAPINZANI
· Asema:Mkinichaguandani yamwaka mmoja kima cha chini cha mshahara kitakuwa laki tatu.
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kwa kuwa ni chama makini kilicho na mipango madhubuti inayotekelezeka na ndio sababu Ilani yake ya uchaguzi imeweza kutekelezwa kwa zaidi ya asilimia tisini.
Amewaeleza maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika kiwanja cha Gombani ya Kale kisiwani Pemba kuwa akichaguliwa tena ataendelea kuweka mazingatio katika suala la kuendeleza amani na utulivu kama alivyofanya katika kipindi kilichopita.
Kwa hivyo aliwakumbusha na kuwaasa wananchi kuacha chokochoko zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani na kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kuwa watu wa Zanzibar ni wamoja hivyo hawapaswi kufarakana badala yake waimarishe udugu wao kwa salama na amani kwa maslahi ya nchi yao.
Dk. Shein alitumia mkutano huo kuielezea Ilani ya CCM katika kipindi kijacho cha uongozi na kuwaeleza wananchi kuwa wanayo kila sababu ya kumuunga mkono yeye na chama chake kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010-2015.
Alibainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake kiwango cha ukuaji wa uchumi kimeongezeka kutoka asilimia 4.3 kwa mwaka hadi asilimia 7.2 hivi sasa wakati mapato ya serikali yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 181.9 mwaka 2010/2011 hadi shilingi bilioni 360.4 mwaka 2014/2015.
Katika kipindi hicho alisema pato la mwananchi mmoja mmoja limeongezeka hadi shilingi milioni 1.56 kwa mwaka.
Kwa mwenendo huo wa uchumi ulioambatana kushuka mfululizo kwa mfumko wa bei alieleza kuwa ni ishara ya mwelekeo mzuri wa uchumi na kuleta matumaini ya kufikia lengo la Dira ya Zanzibar ya kuifanya Zanzibar kuwa nchi yenye uchumi wa kiwango cha kati ifikapo mwaka 2020.
Alisema awamu ijayo kama alivyofanya awamu iliyopita ataongeza kasi ya kuongeza ajira kwa kupanua wigo wa shughuli za kiuchumi ikiwemo kujenga miradi mipya ya kiuchumi itakayotoa ajira nyingi.
Alisisitiza nafasi za ajira hazizuki tu kwa ahadi hewa bali ni mipango mizuri inayotekelezeka na kufanikishwa kwa ufanisi jambo ambalo linaweza kutekelezwa na serikali inayoongozwa na CCM.
Dk.shein alikanusha maelezo ya viongozi wa Chama cha Wananchi –CUF kuwa uamuzi wa kupandisha bei ya karafuu ulifanywa na chama hicho na kuwataka wananchi kutowasikiliza viongozi wa aina hiyo wanaofanya ulaghai katika kuomba kura.
Endapo akichaguliwa, Dk. Shein aliahidi kuongeza kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi 150,000 za sasa hadi shilingi 300,000.

No comments:

Post a Comment