Mgeni rasmi ambae
pia ni makamo wa pili wa rais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar Mh: baozi Seif ali iddi akitoa maelezo machache katika kuwanadi wagombea wa chama cha
mapinduzi katika mkutano wa kwanza uliofanyika tawi la miembeni jitini jimbo la
kikwajuni vile vile akielezea baadhi ya changamoto za kijamii zilizofanyiwa
ufumlbuzi kama kukamilika mradi wa maji safi na salama.
Mh:balozi
akimtambulisha mgombea ubunge kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ENG: hamad yussuf masauni pamoja na
kumkabizi ilani ya chama cha mapinduzi,
ENG: Hamad Yussuf MasaunI
akitoa maelezo mafupi juu ya kuitumikia na kuilinda ilani ya chama cha
mapinduzi.
akiendelea kwa kauli
ya kuwataka wanachama na wakereketwa wa chama cha mapinduzi na wananchi wote
pamoja na wapenda maendeleo kwa ujumla kuwataka kumchagua na kumpa kura ya ndio
ili amalizie kukamilisha miongoni mwa ahadi alizokwisha kuzianza na kulitumikia
jimbo la kikwajuni.
vile vile ENG: Masauni alitoa ufafanuzi juu ya suala la
mradi wa maji katika maeneno ambayo yanasumbuliwa na kutoka kwa maji machafu.
aliwaeleza kuwa
tayari ameshafanya mawasiliano na mamlaka ya maji (ZAWA) na wako mbioni
kulitatuo tatizo hilo. kwani miongoni mwa ahadi zake ni kutatua tatizo la maji
katika jimbo la kikwajuni.
alisema hivyo ili
kukamilisha changamoto hizo nilazima wananchi kuweza kumchagua katika uchaguzi
mkuu october 2
MH: Balozi Seif Ali Iddi
akiwataka wananchi wa jimbo la kikwajuni kumtambua mgombea uwakilishi katika
tiketi ya ccm kuwafikishia matakwa ya wanajamii katika ukumbi wa kutatua
matatizo (baraza la wawakilishi) .
mgombea uwakilishi
huyo akiwa ni mwingi wa furaha baada ya kupokewa vyema na wanachama wa ccm
jimbo la kikwajuni akiahidi kufanya mazuri kwa kuitendea hati ilani ya chama
cha mapinduzi.
wanachama na wapenda
maendeleo wanaogombania udiwani wakiahidi kuitumikia ccm na kuilinda ilani ya
chama baada ya kukabidhiwa rasmi na Mh: Balozi.
ENG: Masauni ni mmoja
kati ya mpenda vijana na kushirikiana nao katika kukamilisha shughuli za
kimaendeleo katika jimbo lake. vijana wakimkubali na kuwanae bega kwa bega.
shamra na shereko
shereko zikitanda katika eneo la mkutano huo baada ya kumalizika kwa mkutano
huo na kuondoka kwa mgeni rasmi na ndipo eng: hamad masauni akijumuika na
vijana wake katika shangwe ya kumainisha ushindi wa kishindo wa tarehe 25
october. vijana wa jimbo la kikwajuni wakionekana kumbeba na kumrusha rusha
kipenzi chao na kidume mleta maendeleo katika jimbo lao.
(PICHA NA MOHAMED
HEMED: BIZO)
No comments:
Post a Comment